Waziri wa Uchumi wa Ujerumani kuwasilisha barua ya kujiuzulu | Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili | DW | 09.02.2009
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Timu Yetu

Waziri wa Uchumi wa Ujerumani kuwasilisha barua ya kujiuzulu

Waziri wa Uchumi wa Ujerumani Michael Glos amesema kuwa atawasilisha hii leo kwa Kansela Angela Merkel barua ya kujizulu.

Michael Glos

Michael Glos

Hatua hiyo inafuatia mkutano uliyokuwa na mzozo kati yake na kiongozi wa chama cha Christian Social Union CSU Horst Seenhofer mjini Munich.


Waziri huyo wa Uchumi wa Ujerumani mwenye umri wa miaka 64 aliomba kujipumzisha kutokana na umri wake na kukitaka chama hicho cha CSU kujitizama upya.


Vyombo vya habari vya hapa Ujerumani vimetabiri ya kwamba huenda Waziri wa fedha wa Jimbo la Bavaria Georg Fahrenschon au Katibu Mkuu wa Chama cha CSU Karl Theodor zu Guttenberg.


Kutoelewana huko katika serikali ya shirikisho la Ujerumani kumekuja mnamo wakati ambapo uchumi wake unakabiliwa na mtikisiko mkubwa kuwahi kuikumba toka kumalizika kwa vita kuu ya pili ya dunia na pia miezi saba tu kabla ya uchaguzi mkuu.


Ujerumani ndiyo yenye uchumi mkubwa kabisa barani Ulaya

LINK: http://www.dw-world.de/dw/article/0,,4012222,00.html

 • Tarehe 09.02.2009
 • Mwandishi Aboubakary Jumaa Liongo
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/GpmI
 • Tarehe 09.02.2009
 • Mwandishi Aboubakary Jumaa Liongo
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/GpmI
Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com