1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Watu waruhusiwa kutembea nje kwa mara ya kwanza Uhispania

Sekione Kitojo
3 Mei 2020

Wahispania waliingia mitaani siku ya Jumamosi kufanya mazowezi ya kukimbia mitaani, kupanda baisikeli  na  michezo mingine  kwa mara ya kwanza  kufuatia  siku 48 za kulazimika  kubakia  majumbani mwao.

https://p.dw.com/p/3bhmy
Spanien Coronavirus Lockerung Ausgangssperre
Picha: Getty Images/C. Alvarez

Wakati huo huo baadhi ya  mataifa ya Ulaya  kwa tahadhari yalilegeza vizuwizi vya kutoka nje, wakati Urusi na Ujerumani zimeripoti ongezeko la maambukizi. Wakati serikali zikitafakari kuondoa vizuwizi vya  kuwataka  wananchi  kubakia  majumbani ili kuanzisha tena  uchumi wao, maafisa nchini Marekani  wameleta  matumaini kiasi  kwa  kuidhinisha  dawa ya  majaribio  ili  itumike  kwa wagonjwa  wa ugonjwa wa  COVID-19.

Spanien Madrid | Coronakrise | Kinder dürfen wieder raus
Watu wameanza tena kuingia mitaani mjini Madrid baada ya kuondolewa vizuwizi vya kukaa majumbani kutokana na virusi vya coronaPicha: picture-alliance/dpa/J. C. Rojas

Uamuzi  huo  ulikuwa  wa  hivi  karibuni  kabisa   katika  hatua  za dunia  kutafuta  dawa  na  chanjo  kwa ajili  ya  virusi  vya  corona, ambavyo  vimesababisha  nusu  ya  binadamu  dunia kuwamo  katika  vizuwizi vya  kutoka  nje na  kuuweka  uchumi  wa  dunia  kuelekea katika  mporomoka  mbaya  kabisa  tangu mdororo  mkuu  katika miaka  ya  1930. Virusi  sasa  vimewauwa  zaidi  ya  watu 242,000 duniani  kote, kwa  mujibu wa  idadi  iliyowekwa  pamoja  na  shirika la  habari  la  AFP, na  walioambukizwa  wanafikia  milioni 3.4  tangu kuzuka  mara  ya  kwanza  virusi hivyo nchini  China mwishoni  mwa  mwaka jana.

Kukiwa na  ishara  kwamba  janga  hili  linapungua  kasi  katika mataifa  yale yaliyoathirika zaidi , mataifa  ya  Ulaya  pamoja  na baadhi  ya  sehemu  za  Marekani  yameanza  kuondoa  vizuwizi kujaribu kurejesha  hali  ya  maisha  kuwa  ya  kawaida  katika uchumi  ambao ulioathirika  kutokana  na  wiki  kadhaa  za kufungwa.

Spanien Madrid | Coronavirus
Mtoto akipanda baisikeli yake karibu na mfanyakazi anayeweka dawa katika maeneo ya nje ya mjini Madrid kuuwa virusi vya coronaPicha: Getty Images/AFP/G. Bouys

Watu watembea mitaani

Kuanzia  Madrid  hadi Mallorca, Wahispania  walimiminika  mitaani baada  ya  kuruhusiwa  kufanya  mazowezi na  kutembea  huru  nje baada  ya  serikali  kulegeza wiki  saba za  udhibiti  mkubwa  wa kuwataka  wananchi  wake  kubakia majumbani  katika  nchi  hiyo iliyokuwa  na  moja  ya  idadi  ya  juu  kabisa  ya  vifo  vilivyofikia zaidi  ya  25,000. "Baada  ya  wiki  kadhaa za  kufungiwa, nilikuwa nahitaji  sana  kutembea  nje, kukimbia, na  kuona  dunia," alisema mshauri  wa   masuala  ya  fedha Marcos Abeytua  mjini  Madrid. "Jana  nilikuwa  kama  mtoto  katika  mkesha  wa  krismass."

Uhispania, Ujerumani, Austria na  mataifa  ya  Scandinavia taratibu yanalegeza  vikwazo vya  kuwazuwia  watu  kutoka  majumbani, wakati  kesi  za  virusi  vya  corona  zikipungua licha ya  kuwa  hatua za  watu  kukaa  mbali  mbali  zitaendelea, matumizi  ya barakoa pamoja  na  uchunguzi  kujaribu  kufuatilia  maambukizi.

Coronavirus Spanien Madrid Verteilung von Mundschutz
Polisi akigawa barakoa mjini Madrid baada ya wakaazi wa mji huo kuruhusiwa kutoka nje kwa mara ya kwanza , Jumamosi (02.05.2020)Picha: Imago Images/Zuma/B.G. Rouco

Ufaransa, ambayo itaondoa  sehemu ya  vizuwizi  vya  kutotembea nje hapo Mei 11, jana Jumamosi (02.05.2020) ilirefusha  hali ya dharura ya kiafya  kwa  miezi miwili  zaidi hadi  mwishoni  mwa  Julai wakati  ikiripoti  vifo vipya  166,  ikiwa  ni idadi ya chini  kabisa  ya vifo  katika  zaidi  ya  wiki tano.

Idadi  ya kesi  zilizothibitishwa za  virusi  vya  corona nchini  Ujerumani imeongezeka kwa watu 793 na  kufikia 162,496, ikiwa  ni  data kutoka  taasisi  ya  kupambana  na  magonjwa  ya  kuambukiza  ya Robert Koch RKI , leo  Jumapili (03.05.2020).

Idadi  ya  vifo  vilivyoripotiwa  imepanda  kwa watu 74  na  kufikia vifo 6,649 kwa jumla.