Watu 20 Ujerumani kwa kusafirisha watu kwa magendo | Habari za Ulimwengu | DW | 18.12.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Watu 20 Ujerumani kwa kusafirisha watu kwa magendo

BERLIN

Maafisa wa serikali ya Ujerumani wamewakamata watu 20 katika uchunguzi wa kundi linalotuhumiwa kuwasafirisha kwa magendo vijana wa kike wa Nigeria barani Ulaya kufanya kazi za ukahaba.

Ofisi ya Jinai ya serikali ya Ujerumani imesema katika taarifa kwamba watuhumiwa hao walikamatwa Alhamisi iliopita na Ijumaa huko Frankfurt.Ofisi hiyo imesema kwamba imekuwa ikichunguza tokea mwezi wa April kundi hilo la Wajerumani na Wanigeria.

Polisi imesema kundi hilo limekuwa likiandaa kuwasafirisha kwa magendo raia wa Nigeria wengi wakiwa ni wanawake wenye umri wa chini ya miaka 21 kuja Ulaya kufanya kazi katika biashara ya ngono.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com