Watu 18 wauwawa Iran kwa mashambulizi ya Israel
7 Aprili 2026
Shirika la habari la Fars limeripoti, kuuwawa kwa takriban watu 18 na 24 wamejeruhiwa, kufuatia mashambulio ya anga ya Israel yaliyofanywa dhidi ya eneo la makaazi ya watu katika mkoa wa Alborz nchini Iran.
Vyombo vya habari vya Iran pia vimeripoti kuhusu miripuko kadhaa iliyosikika mjini Tehran leo na Iran ikifyetuwa makombora kuelekea mji wa Tel Aviv,Israel na Saudi Arabia na kufunga kwa muda daraja lake kubwa.Majengo kadhaa yameharibiwa Tel Aviv, kwa mujibu wa Televisheni ya Israel.
Marekani, Israel zazidi kuwaangamiza makamanda wa IRGC
Maafisa wa Iran wametowa mwito kwa vijana nchini humo kuungana kuilinda mitambo ya nishati nchini humo kwa kuizunguuka, wakati muda wa mwisho wa saa mbili usiku, uliotolewa na rais Donald Trump, kuilazimisha Iran ifungue mlango bahari wa Hormuz ukikaribia.
Uingereza yaongoza mkutano wa kujadili kufunguliwa kwa Hormuz
Trump ametishia kushambulia mitambo yote ya nishati na madaraja nchini Iran baada ya utawala wa jamhuri ya Kiislamu mjini Tehran kukataa pendekezo la kusitisha vita kwa siku 45 ikisema inataka mpango wa kudumu wa kumaliza vita.
Marekani, Israel zazidi kuwaangamiza makamanda wa IRGCMarekani, Israel zazidi kuwaangamiza makamanda wa IRGC