Watibet wawe na uhuru wa dini na kitamaduni | Habari za Ulimwengu | DW | 15.03.2008
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Watibet wawe na uhuru wa dini na kitamaduni

BERLIN:

Kufuatia machafuko yaliyozuka kati ya waandamanaji na polisi katika mji mkuu wa Tibet-Lhasa,Kansela wa Ujerumani Angela Merkel ametoa wito wa kujizuia kwa pande zote mbili.Wakati huo huo,msemaji wake mjini Berlin amesisitiza haki ya Watibet kuwa na uhuru wa dini na kitamaduni.Uhusiano kati ya Ujerumani na China uliingia katika hali ya mvutano baada ya kiongozi wa kidini wa Tibet Dalai Lama kupokewa na Kansela Merkel mjini Berlin,Septemba mwaka 2007.

Siku ya Ijumaa,maandamano ya kupinga utawala wa China katika Tibet yaligeuka kuwa machafuko,baada ya vikosi vya usalama vya China kujaribu kuyavunja maandamano hayo kwa kuzingira nyumba tatu za watawa mjini Lhasa.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com