Washington. Zoellick rais mpya wa benki kuu ya dunia. | Habari za Ulimwengu | DW | 31.05.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Washington. Zoellick rais mpya wa benki kuu ya dunia.

Rais wa Marekani George W. Bush amemtangaza mwakilishi wa zamani wa biashara nchini Marekani Robert Zoellick kuwa rais mpya wa benki ya dunia.

Bush ametoa tangazo hilo katika mkutano na waandishi wa habari katika Ikulu ya Marekani.

Zoellick amedokeza kuwa anataka kujenga upya heba ya taasisi hiyo ya kimataifa baada ya rais wa sasa wa benki kuu ya dunia Paul Wolfowitz kutuhumiwa kuhusika katika kashfa ya malipo na kumpandisha cheo mpenzi wake wa kike.

Uteuzi wa Zoellick unahitaji hata hivyo kuidhinishwa na bodi ya magavana wa benki hiyo yenye wanachama 24.

Paul Wolfowitz amekubali kujizulu mwishoni mwa mwezi Juni baada ya jopo maalum kugundua kuwa alivunja sheria za benki hiyo kwa kupanga kiasi kikubwa cha fedha kama fidia kwa mpenzi wake mwaka 2005.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com