1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

WASHINGTON: Wolfowitz apambana na wito wa kujiuzulu

10 Mei 2007
https://p.dw.com/p/CC3n

Marekani imesisitiza kuwa inamuunga mkono rais wa Benki Kuu ya Dunia Paul Wolfowitz,huku nchi za Ulaya zikitoa wito wa kumaliza kwa haraka kashfa inayohusika na madai ya upendeleo.Wolfowitz ambae hapo zamani alikuwa makamu wa waziri wa ulinzi wa Marekani,anapambana na wito mkali,ndani na nje ya Benki Kuu kumtaka ajiuzulu baada ya kufichuliwa kuwa mkuu huyo binafsi,alisaidia kumuongezea mshahara na kutoa ahadi ya kumpandisha cheo mpenzi wake Shaha Riza anaefanya kazi pia katika Benki Kuu ya Dunia.Siku ya Jumatano,katibu katika wizara ya maendeleo ya Ujerumani,Karin Kortmann alisema kuwa waziri Heidemarie Wiezorek-Zeul wakati wa mikutano ya Benki Kuu mwezi wa Aprili alimuambia Wolfowitz kuwa anahofia uaminifu wa benki hiyo na alimhimiza mkuu huyo wa benki ajiuzulu.