1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

WASHINGTON Wanajeshi 11 wa Marekani washtakiwa kwa kuwatesa wafungwa nchini Irak

16 Julai 2005
https://p.dw.com/p/CEu3

Jeshi la Marekani limewashtaki maofisa wake 11 nchini Irak kwa kuwatesa wafungwa wanaotuhumiwa kuwa wapiganaji. Wanajeshi hao walikatwa mnamo Jumatano iliyopita kufuatia ripoti iliyotolewa na mwanajeshi mwingine.

Hata hivyo hakuna habari zaidi zilizotolewa kuhusiana na mateso ya wafungwa hao, lakini imethibitishwa kwamba hawakuumizwa kiasi cha kuhitaji matibabu. Wanajeshi wengi wa Marekani wamehusika katika visa vya mateso ya wafungwa nchini Irak, visa vibaya zaidi vikiripotiwa katika jela ya Abu Ghraib karibu na mji wa Bahgdad.