WASHINGTON: Ombi la bajeti ya Bush lavunja rekodi | Habari za Ulimwengu | DW | 06.02.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

WASHINGTON: Ombi la bajeti ya Bush lavunja rekodi

Rais George W.Bush wa Marekani amewasilisha ombi la bajeti ya dola trillioni 2.9 kwa matumizi ya mwaka mmoja ujao.Matumizi mapya ya kijeshi yanatazamiwa kugharimu zaidi ya dolla billioni 700.Sehemu kubwa ya pesa hizo zimepangwa kutumiwa katika vita vya Irak.Wakati huo huo Bush ameonya kuwa pesa zaidi huenda zikahitajika.Wabunge wa Demokrats lakini wanasema,bajeti iliyopendekezwa itapunguza miradi ya nyumbani ikiwa ni pamoja na ile inayohusika na afya na elimu.Wakati huo huo Wademokrats wamesema kuwa watachunguza matumizi yanayohusika na vita vya Irak,lakini wameahidi kutopunguza pesa kwa ajili ya vikosi vya Kimarekani ambavyo tayari vipo nchini Irak.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com