WASHINGTON: Olmert amewasili Marekani kwa mazungumzo na Bush | Habari za Ulimwengu | DW | 12.11.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

WASHINGTON: Olmert amewasili Marekani kwa mazungumzo na Bush

Waziri mkuu wa Israel,Ehud Olmert amewasili Washington nchini Marekani kwa mkutano wake wa pili pamoja na rais George W.Bush.Mkutano huo umepangwa kufanywa siku ya Jumatatu.Kufuatia matokeo ya hivi karibuni ya uchaguzi wa bunge nchini Marekani,Olmert amesema anataka kujiarifu juu ya siasa ya Washington kuhusu mgogoro wa Waisraeli na Wapalestina.Suala la Iran pia linatarajiwa kuchukua nafasi muhimu katika mazungumzo ya viongozi hao wawili.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com