WASHINGTON: Mwanajeshi wa Marekani ahukumiwa miaka 100 jela | Habari za Ulimwengu | DW | 23.02.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

WASHINGTON: Mwanajeshi wa Marekani ahukumiwa miaka 100 jela

Mahakama ya kijeshi nchini Marekani imemhukumu mwanajeshi mmoja wa Marekani kifungo cha miaka 100 gerezani kwa makosa ya ubakaji na mauaji ya msichana wa umri wa miaka 14. Mwanajeshi huyo pia alipatikana na makosa ya kuiua familia yote ya msichana huyo katika mji wa Mahmudiyah nchini Irak mwaka mmoja uliopita.

Sajini Paul Cortez mwenye umri wa miaka 24 alikuwa amekiri kufanya makosa hayo wakati alipokata rufaa. Aliiambia mahakama hiyo katika jimbo la Kentucky kwamba alikuwa miongoni mwa wanajeshi watano waliokula njama kufanya ubakaji huo na mauaji hayo wakati walipokuwa wakinywa pombe na kucheza karata.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com