WASHINGTON: Daktari wa upasuaji katika hospitali ya kijeshi ajiuzulu | Habari za Ulimwengu | DW | 13.03.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

WASHINGTON: Daktari wa upasuaji katika hospitali ya kijeshi ajiuzulu

Daktari mkuu wa upasuaji wa jeshi la Marekani amejiuzulu kufuatia kashfa katika hospitali ya kijeshi ya Marekani ya Walter Reed. Luteni jenerali Kevin Kiley ni kiongozi wa tatu wa cheo cha juu kupoteza kazi yake kufuatia habari kwamba wanajeshi wanaojeruhiwa nchini Irak na Afghanistan hawapati matibau mazuri katika hospitali hiyo.

Ripoti za hivi karibuni zilizotolewa na magazeti ya Marekani zilieleza hali mbaya katika hospitali hiyo, ikiwa ni pamoja na vyumba vilivyojaa panya na mende.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com