Waasi 5 wa FNL wauwawa kwenye mapigano na jeshi | IDHAA YA KISWAHILI | DW | 10.01.2008
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

IDHAA YA KISWAHILI

Waasi 5 wa FNL wauwawa kwenye mapigano na jeshi

---

BUJUMBURA

Waasi watano wa kundi la FNL Palipehutu nchini Burundi waliuwawa na wanajeshi watatu wakajeruhiwa hapo jana katika mapigano makali kuwahi kutokea kati ya jeshi la serikali na waasi hao tangu kusitishwa mapigano mwaka 2006.

Duru za kijeshi nchini humo zimefahamisha kwamba kiasi cha waasi 40 wa FNL walivamia kituo cha jeshi katika eneo la Kirari wilayani Musigati na kusababisha mapambano makali.Kundi la FNL ni kundi pekee la waasi lililosalia nchini Burundi na limekataa kutekeleza makubaliano ya amani na serikali yaliyotiwa saini septemba 2006 baada ya kujitoa kwenye mazungumzo ya amani july mwaka jana.Wakati huohuo waziri wa mambo ya nje wa China Yang Jiechi yuko nchini Burundi kwa ziara yenye malengo ya kufunga mikataba ya kibiashara na taifa hilo.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com