Virusi vya aina mpya ya Ebola vimeua watu 2 wengine Uganda | Habari za Ulimwengu | DW | 01.12.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Virusi vya aina mpya ya Ebola vimeua watu 2 wengine Uganda

Watu 2 wengine wamefariki nchini Uganda kutokana na aina mpya ya virusi vya homa ya Ebola vilivyoripuka karibu na mpaka wake na Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo.Mkurugenzi wa Huduma za Afya nchini Uganda,Sam Zaramba amesema,sasa idadi ya watu waliofariki kwa ugonjwa huo imefikia 18. Akaongezea kuwa maafisa wa Shirika la Afya Duniani-WHO wanashirikiana na wataalamu wa Uganda kupanga mkakati wa kuzuia ugonjwa huo kutoka nje ya eneo la Bundibugyo magharibi mwa nchi.Hadi watu 51 wameambukizwa virusi hivyo ambavyo ni vya aina mpya ya homa ya Ebola.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com