1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Viongozi wa G7 wawasili Canada kwa mkutano wa kilele

16 Juni 2025

Kundi la viongozi wa mataifa saba tajiri kiviwanda G7, wamewasili tangu jana nchini Canada kwa ajili ya mkutano wa kilele.

https://p.dw.com/p/4vxva
Canada G7 Kananaskis 2025 | Mkutano wa kilele wa viongozi wa G7
Mkutano wa kilele wa viongozi wa G7 mjini Kananaskis Picha: Todd Korol/REUTERS

Kundi la viongozi wa mataifa saba tajiri kiviwanda G7, wamewasili tangu jana nchini Canada kwa ajili ya mkutano wa kilele na kuona ikiwa watatoka na msimamo wa pamoja kuhusu mzozo unaoendelea kati ya Israel na Iran. 

Mkutano huo wa siku tatu katika mji wa mlima wa Kananaskis unaashiria kurudi kwa Rais Donald Trump katika mikutano ya kimataifa, ambaye katika muhula wake wa pili amekuwa na ujasiri zaidi wa kuvunja kanuni za jadi.

Waziri Mkuu wa Canada Mark Carney alikuwa ameandaa ajenda inayolenga kupunguza tofauti ndani ya kundi hilo la mataifa tajiri kiviwanda, ya Uingereza, Canada, Ufaransa, Ujerumani, Italia, Japan na Marekani.

Viongozi hao wa G7 wanaweza kushuhudia mgawanyiko kuhusu mgogoro wa sasa kati ya Israel na Iran.