1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Biashara

EU kukamilisha makubaliano ya biashara huria na India

26 Januari 2026

Viongozi wa Umoja wa Ulaya wameungana na viongozi wa India katika gwaride la kuadhimisha siku ya Jamhuri ya India leo. Hafla hiyo inafanyika siku moja kabla ya kukamiliswha kmakubaliano ya muda mrefu ya biashara huria.

https://p.dw.com/p/57Sta
India New Delhi 2026 | Modi akisalimiana na von der Leyen katika gwaride la Siku ya Jamhuri
Waziri Mkuu wa India Narendra Modi akisalimiana na Rais wa Halmashauri ya Umoja wa Ulaya Ursula von der LeyenPicha: Adnan Abidi/REUTERS

Viongozi wa Umoja wa Ulaya wameungana na viongozi wa India katika gwaride la kuadhimisha siku ya Jamhuri ya India leo. Hafla hiyo inafanyika siku moja kabla ya pande hizo mbili kukamilisha makubaliano ya muda mrefu ya biashara huria.

Rais wa Baraza la Ulaya, Antonio Costa na Rais wa Halmashauri ya Umoja wa Ulaya, Ursula von der Leyen, wanahudhuria hafla hiyo, kabla ya mkutano wa kilele kati ya Umoja wa Ulaya na India utakaofanyika kesho Jumanne, ambapo pande hizo mbili zinatarajiwa kutangaza mkataba muhimu wa biashara huria pamoja na ushirikiano wa kiusalama.

India na Umoja wa Ulaya zimekuwa zikijadiliana juu ya makubaliano ya biashara kwa zaidi ya muongo mmoja kabla ya ushuru wa kibiashara uliowekwa na Rais wa Marekani Donald Trump kuzisukuma pande hizo kuharakisha juhudi zao mwaka jana.