1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Umoja wa Ulaya walaani kitisho cha Trump kwa NATO

Sudi Mnette
12 Februari 2024

Rais wa Baraza la Umoja wa Ulaya, Charles Michel amekiita kitishio cha Rais wa Zamani wa Marekani Donald Trump kwa wanachama wa NATO wanaolegalega katika michango kutowailinda kuwa kisicho na maana yoyote.

https://p.dw.com/p/4cHFi
Rais wa Baraza la Umoja wa Ulaya, Charles Michel
Rais wa Baraza la Umoja wa Ulaya, Charles Michel akizungumza na waandishi wa habari alipowasili kuhudhuria mkutano wa kilele wa Umoja wa Ulaya katika makao makuu huko Brussels, Desemba 13, 2023Picha: Kenzo Tribouillard/AFP

Rais wa Baraza la Umoja wa Ulaya, Charles Michel amekiita kitishio cha Rais wa Zamani wa Marekani Donald Trump kwamba endapo atakachuguliwa tena kuwa rais hatozilinda nchi za Jumuiya ya NATO ambazo hazitowajibika vyema katika uchangiaji wa jumuiya hiyo kuwa ni uzembe. Kupitia ukurawa wake wa X, zamani Twitter, Michel amesema kwa takribani miaka 75  jumuiya hiyo imekuwa na jukumu la kuimarisha usalama na ustawi wa Wamarekani, watu wa Ulaya hadi Canada kwa kipindi chote hicho.Aidha ameongeza kwa kusisitiza tena uhitaji wa Ulaya kuendelea kwa kasi zaidi katika mkakati na kuwekeza katika ulinzi wake. Jumamosi iliyopita Trump alitoa kitisho cha kwamba  iwapo atachaguliwa tena nchini Marekani, hatawatetea wanachama wa NATO ambao hawajatimiza wajibu wao wa kifedha, na kwenda umbali zaidi kwa kutoa kauli iliyoonesha kama akihimiza Urusi kuwashambulia.