1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroUlaya

Ukraine kuwasilisha nyaraka ya mpango wa amani uliyoboreshwa

10 Desemba 2025

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky amesema anatarajia Jumatano kuwasilisha kwa Marekani, nyaraka ya mpango wa amani ambayo imefanyiwa marekebisho kwa usaidizi wa washirika wake wa Ulaya.

https://p.dw.com/p/552ek
Kiev 2025 | Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky akizungumza na wanahabari
Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky akizungumza na waandishi wa habari mjini KievPicha: Tetiana Dzhafarova/AFP

Mwishoni mwa mwezi Novemba, utawala wa rais wa Marekani Donald Trump ulipendekeza mpango wa amani uliokosolewa vikali na Ukraine pamoja na washirika wake wa Ulaya kwa kuwa uliitaka Ukraine kuachia baadhi ya sehemu ya ardhi yake kwa Urusi.

Aidha Zelensky ameongeza kuwa yuko tayari kuandaa uchaguzi mpya nchini Ukraine ikiwa watahakikishiwa usalama huku akisisitiza kuwa Urusi haioneshi nia ya kuendelea na  mchakato wa amani , kwani inaendeleza mashambulizi makali dhidi ya miundombinu yake ya nishati.