MigogoroUlaya
Shambulio la kisu lazusha vurugu Ireland Kaskazini
10 Juni 2026
Matangazo
Shirika la Habari la AFP limeripoti kwamba mamia ya waandamanaji waliojifunika nyuso walikusanyika kwenye maeneo kadhaa ya mji wa Belfast wakirusha mabomu ya petroli na kufunga barabara.
Basi la abiria na magari kadhaa yamechomwa moto huku jengo moja nalo lilishika moto na kulazimisha wakaazi wake kuondolewa. Tukio lililochochea vurumai hiyo lilirekodiwa kwenye video na taarifa zinasema mtuhumiwa wa shambulio hilo kisu tayari amefunguliwa mashtaka ya kujaribu kuua.
Wanasiasa na wanaharakati wanaopinga uhamiaji wanataka jina lake litajwe baada ya wizara ya mambo ya ndani kuthibitisha anayetuhumiwa ni mhamiaji kutoka nchini Sudan.