Ujerumani yataka kuwajumulisha wahamiaji katika mfumo wake | Masuala ya Jamii | DW | 18.02.2008
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Masuala ya Jamii

Ujerumani yataka kuwajumulisha wahamiaji katika mfumo wake

Mila na desturi za baadhi ya wahamiaji zinapingana na za Ujerumani

Ujerumani, mmoja wa nchi zenye viwanda vingi duniani,inakabiliwa na changamoto ya kuwa na idadi kubwa ya watu wanaozeka.Na tatiza ni jinsi ya kuwajumulisha wazee ambao wengi ni wahamiaji.

Kwa mda mrefu,maafisa wa utawala nchini Ujerumani walidhani kuwa wafanya kazi wa kigeni ambao waliajiriwa baada ya vita vikuu vya pili vya dunia,watarejea nyumbani kwao wakimaliza kibarua chao.

Lakini sasa inaonekana ndoto zao hazikutimilizika,kwani wakazi wake wapatao millioni 2 unusu wenye asili ya kituruki hawabanduki,na idadi kubwa ya watu hao inakaribia umri wa kustaafu.

Afisa mmoja wa shirika la misaada ya kiutu la Caritas-Ulrika Zabel- amenukuliwa akisema kuwa ,kwa mda mrefu Ujerumani haikudhani kuwa itakuwa mojawapo wa nchi ya wahamiaji.Shirika hilo ,kwa ushirikiano na lingine la kibinafsi linalotoa makazi kwa watu wa umri mkubwa-Vitanas,litafungua kituo cha nne cha makazi ya wazee mjini Berlin mwaka ujao.

Ameongeza kuwa kwa sababu waliotangulia hawakutaraji kuwa wahamiaji hawa wangekaa hapa Ujerumani milele na milele kumetokea matatizo fulani.

Mfano Baba wa mmoja,mwenye Umri wa miaka 68 sasa, alikuja Ujerumani mwaka wa 1973 kutoka Uturuki.Mipango yake wakati huo ilikuwa kufanya kazi hapa Ujerumani kwa kipindi cha miaka mitano tu.Lakini ameendelea kukaa akifanya kati kama makanika wa mashine katika kampuni ya Siemens kwa miaka 25.

Licha ya kuwa na nyumba nyumbani Uturuki,mzee huyo ambae sasa amestaafu,bado hukaa karibu nusu ya mwaka mjini Berlin.

Mtoto wake Mustafa Makinist ,mwenye umri wa miaka 40,anapanga kukodisha nyumba mjini Berlin ambayo itatumiwa na wazazi wake mama na baba wakifikia umri mkubwa sana ambao hautawawezesha kusafiri katika nyumba asili ya Uturuki na nyumba yao mpya yaani Ujerumani. Lakini amekanusha dhana eti jamii za Kituruki,huishi katika nyumba moja kubwa ,mtoto,mama,watoto, wazee,wajukuu na kadhalika.

Amesema kuwa kizazi cha pili kimechukua mila za kijerumani na pia nyumba za mjini Berlin ni ndogo kuweza kutosha watu wengi.

Juhudi za serikali ya Berlin za kuwajumuisha watu wa tabaka,mila na desturi za kigeni kufuata maadili ya kijerumani sanasana kutokana na hofu ya usalama,mkazo umepewa kuwasaidia vijana.

Hata hivyo baadhi ya mashirika yameanza kukimulika kizazi ambacho ndio sasa kinakaribia miaka ya kustaafu. Na makampuni mengi yemanza kujitafutia wateja.

Takwim zilizotolewa mwaka wa 2006 na ofisi ya shirikisho inayohusika na takwimu,zinaonyesha kuwa karibu asili mia 18 ya wahamiaji wa Ujerumani ni wa umri wa miaka inayozidi 55. Zaidi ya laki saba ya wahamiaji wenye makamo wako katika muongo wa mwisho wa kipindi chao cha kufanya kazi wakiwa wanausogelea ule mda wa kufuzu kupata malipo ya uzeeni.

Taarifa za hivi punde za Ujerumani kuhusu uzee zilichapishwa mwaka wa 2005.Katika taarifa hiyo ilidhihirika kuwa wahamiaji wazee litakuwa mmoja wa mikakati itakayopewa uzito na serikali.

Ripoti iligundua kuwa wahamiaji wazee wanakabiliwa mno na matatizo ya kiafya,kipato cha chini na pia elimu duni kuhusu kuwepo huduma za jamii kuliko wenzao wa kijerumani.

Wahamiaji ambao wameishi Ujerumani kwa mda unaozidi miaka 25 wamesaidia kuchangia serikali kwa wastani Euro 850 kwa mwaka kwa kila mtu.Na serikali kwa upande wake imetumia takriban Euro millioni 5 kwa mipango inayowahusu wahamiaji wazee.

Wahamiaji wazee,kinyume na wenzao wajerumani,wanawezekana wasipate mafao,ingawa wanafuzu kupewa ikiwa walichangia katika mfuko wa umma.

Ripoti hiyo pia iligundua kuwa mnamo mwaka wa 2002,takriban asili mia 79 ya wahamiaji wa kituruki walio na umri wa miaka zaidi ya 65,ilikuwa inapokea mafao yao ikilinganishwa na takriban asili mia 96 ya wenzao wajerumani asili.

Hata hivyo tofauti ya mila na tamaduni huenda ikawa kikwazo cha iana fulani katika mpango mzima wa kuwafanya wageni kujumuishwa nchini Ujerumani.

Limegusiwa suala la kuwa wahamiaji wa kituruki ama kiarabu huwa na familia kubwa.

Lakini katika maisha ya kawaida ya vituo vya makazi ya wazee vya Kijerumani, si kawaida mtu kutembelewa na watu wake kila mara, huwa ni wakati wa Krismasi au Pasaka.

 • Tarehe 18.02.2008
 • Mwandishi Kalyango Siraj
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/D9NR
 • Tarehe 18.02.2008
 • Mwandishi Kalyango Siraj
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/D9NR
Matangazo

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com