Ujerumani yasema haina nia ya kutuma vikosi zaidi nchini Afghanistan | Habari za Ulimwengu | DW | 01.02.2008
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Ujerumani yasema haina nia ya kutuma vikosi zaidi nchini Afghanistan

WASHINGTON:

Wizara ya Ulinzi ya Ujerumani imeeleza kuwa waziri wa ulinzi wa Marekani-Robert Gates amemwandikia barua waziri mwenzake wa Ujerumani kutuma wanajeshi zaidi 3,200 nchini Afghanistan.Gates ameonya kuwa majeshi ya NATO yanaweza kupoteza heshima yake ikiwa majeshi hayataongezwa.Mwito wa waziri wa ulinzi wa Marekani unakuja wakati kukishuhudiwa kuongezeka kwa mashambulizi ya waasi nchini Afghanistan.Yeye balozi wa Uingereza nchini Afghanistan –Sherard Cowper –Coles anasema ghasia nchini humo zinatokea katika sehemu ndogo nchini humo.

Katika barua kwa waziri wa Ulinzi wa Ujerumani- Franz Josef Jung,Gates hususan ameitaka serikali ya Ujeruamni kutafuta uwezekano wa kupata ruhusa mpya wa bunge la nchi hiyo kwa ajili ya kujiunga na mapambano dhidi ya wapiganaji wa Taliban wa upande wa kusini.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com