1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ujerumani yaongeza msaada wake kwa Pakistan

Aboubakary Jumaa Liongo15 Agosti 2010

Ujerumani imeongeza msaada wake kwa wahanga wa mafuriko nchini Pakistan kutoka Euro millioni 5 hadi millioni 15.Fedha hizo zitatumika kwa ajili ya maji ya kunywa, madawa pamoja na chakula.

https://p.dw.com/p/OnzM
Wahanga wa mafuriko PakistanPicha: AP

Waziri wa Maendeleo wa Ujerumani Dirk Niebel amesema msaada wa haraka kutoka jumuiya ya kimataifa ni jambo muhimu ili kuwazuia Waislamu wenye itikadi kali pamoja na kundi la Taliban kusambaza ushawishi wao miongoni mwa watu wanaoteseka nchini Pakistan.

Waziri Mkuu wa Pakistan Yousuf Raza Gilani ameiomba jumuiya ya kimataifa msaada zaidi akisema kuwa mafuriko hayo yameharibu akiba ya chakula pamoja na mazao.

Wakati huo huo watu kiasi ya millioni 20 wameathiriwa na mafuriko hayo.Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon hii leo anatarajiwa kutembelea maeneo yaliyokumbwa na janga hilo.

Mwandishi:Aboubakary Liongo

Mhariri:Prema Martin