1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mwanadiplomasia wa Urusi aitwa serikalini Ujerumani

4 Mei 2024

Ujerumani imemwita kwa mahojiano kaimu kiongozi katika masuala ya nje wa Urusi katika ubalozi wa taifa hilo nchini Ujerumani kwa kumtaka kujibu tuhuma za shambulio la mtandaoni la Urusi la mwaka uliopita.

https://p.dw.com/p/4fUv4
Rais Putin wa Urusi
Rais wa Urusi Vladimir Putin akitoa hotuba ya video kwa taifa, Machi 23, 2024,Picha: Kremlin.ru/REUTERS

Ujerumani imemwita kwa mahojiano kaimu kiongozi katika masuala ya nje wa Urusi katika ubalozi wa taifa hilo nchini Ujerumani kwa kumtaka kujibu tuhuma za shambulio la mtandaoni la Urusi la mwaka uliopita kwa chama kilicho katika hatamu ya uongozi cha Social Democratic (SPD).

Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya Ujerumani akiwa mjini Berlin amesema afisa huyo mwandamizi, Alexei Korlyakov, alifika katika ofisi mchana ya Ijumaa.

Msemaji huyo ameongeza kwa kusema kidiplomasia hatua hiyo inaonesha wazi kabisa kwa serikali ya Urusi kwamba Ujerumani haikubaliani na kitendo hicho na inakilaani.

Mapema Ijumaa, Umoja wa Ulaya na NATO zilitoa taarifa za kulaani shambulio dhidi ya Ujerumani na Jamhuri ya Czech, ambayo inasema pia ilikuwa iliyolengwa.