1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Intaneti

Intaneti ni mfumo wa dunia wa mitandao huru ya computer. Unaruhusu matumizi ya huduma za computer kama vile World Wide Web (WWW), Email (Barua-pepe) au FTP.

Protolali za intaneti zilizowekwa katika kiwango kinachokubalika kiufundi zinaunda msingi wa mawasiliano ya kimtandao. Kitangulizi cha intaneti ni mtandao wa computer wa APRANET uliotengenezwa na wizara ya ulinzi ya Marekani mwaka 1968. Lengo lilikuwa kuunganisha taasisi za kijeshi na kielimu nchini Marekani. Mtandao wa kwanza ulihusisha computer nne tu kutoka vyuo vikuu mbalimbali ambazo zingeweza kupeleka data kwa kila mmoja wao.Hii leo karibu nusu ya wakaazi wa dunia wanatumia intanet. Kusambazwa kwa intanet kumechangia kuleta mabadiliko katika nyanja zote za maisha.

Onesha makala zaidi