Ujerumani yailaza Uingereza bao nne kwa moja. | Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili | DW | 28.06.2010
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages

Timu Yetu

Ujerumani yailaza Uingereza bao nne kwa moja.

Mashindano ya kombe la dunia ya soka yanaendelea leo nchini Afrika kusini, baada ya timu mbili za Ujerumani na Argentina jana kufanikiwa kuingia robo fainali za mashindano hayo.

default

Vikosi vya Ujerumani na Uingereza vilivyopambana jana.

Mashindano ya kombe la dunia ya soka yanaendelea leo nchini Afrika kusini, baada ya timu mbili za Ujerumani na Argentina jana kufanikiwa kuingia robo fainali za mashindano hayo.

Ujerumani ilifanikiwa kusonga mbele baada ya kuibamiza Uingereza mabao manne kwa moja, ambapo magoli yake yalifungwa na Miroslav Klose na Lukas Podolski katika kipindi cha kwanza na mengine mawili yalifungwa na Thomas Mueller katika kipindi cha pili.

Deutsche Fußballfans in Berlin WM 2010 Flash-Galerie

Washabiki wa timu ya taifa ya soka ya Ujerumani, wakishangilia timu yao, ilipoinyuka Uingereza goli nne kwa moja, hapo jana, nchini Afrika kusini.

Goli la Uingereza la kufutia machozi lilifungwa na Matthew Upson.

Na katika mchezo mwingine uliochezwa hapo jana, Argentina nayo iliweza kusonga mbele kwa kuifunga Mexico, mabao matatu kwa moja.

Argentina itapambana na Ujerumani katika robo fainali, Jumamosi ijayo.

 • Tarehe 28.06.2010
 • Mwandishi Halima Nyanza
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/O4gm
 • Tarehe 28.06.2010
 • Mwandishi Halima Nyanza
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/O4gm

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com