1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ujerumani yachangia Euro bilioni 500

14 Oktoba 2008

Kurejesha utulivu katika soko la fedha,serikali ya Ujerumani inachangia Euro bilioni 500.

https://p.dw.com/p/FYyi
kanzla Angela MerkelPicha: AP

Mpango wa kuyaokoa masoko ya fedha yaliokumbwa na msukosuko nchini Ujerumani, umeshatungwa na kupitishwa. Serikali ya Ujerumani imeamua kuanzisha mfuko wa kitita cha Euro bilioni 500 ili kuimarisha nguvu na uwezo wa mabanki ya Ujerumani.Shabaha ya kuwa na bajeti isio na kasoro baina ya mapato na matumizi ambayo waziri wa fedha wa Ujerumani Bw.Peer Steinbruck akilenga kuifikia ifikapo 2011,sasa imetolewa mhanga kutokana na mpango huo uliopitishwa.Na hii si uzuri kufanya hivyo ,lakini kwa hali ya sasa inahitajika.

Kumimina kitita cha Euro bilioni 500 kukabiliana na hatari iliozuka na hivyo kuikausha hazina ya serikali, ni mawazo ambayo yatasalia vichwani mwa watu.Lakini hatua hiyo ina manufaa yake ukiangalia mipango mbali mbali iliomo ndani ya kifurushi cha hatua za kuyaokoa masoko ya fedha.

Kuna mfuko wa kuimarisha masoko ya fedha ikiwa mali maalumu ya serikali ya shirikisho-mfuko ambao utadhaminiwa kwa hadi Euro bilioni 400.Unawezesha mabanki kujipatia hazina mpya ya fedha kwa kushirikiana na serikali.Kwa mfano serikali inaweza kununua hisa ndani yamabenki hayo.Kwa ajili hiyo kitita cha euro bilioni 80 kimepangwa kutolewa. Kuudhamini mfuko huo kimetengwa kitita cha Euro bilioni 20.Hatua hizi zote zina maana gani ?

Kwanza, neno "hazina maalumu" ya serikali lina maana serikali ghafula inamiliki kitita cha Euro bilioni 400.Kinyume chake, neno "hazina maalumu" lina maana pia kima hicho hakimo kabisa katika mfuko wa matumizi ya serikali na hivyo, hakiwezi kutumika. Ni sawa na kusema hii ni "hazina upepo"-ipo kama haipo na ambayo, haiina hata centi moja ndani yake kwa kutumai kuwa, hakuna Banki ya kijerumani itakayofikia kuhitaji kuomba msaada itiwe jeki na mfuko huo.

Kwa muujibu wa rasimu ya sheria ya hivi sasa, mabenki hayana pia dai la msaada maalumu.Lini na wapi viraka vizibwe,watakaoamua ni wanasiasa.Serikali itatia jeki ikiambatisha masharti maalumu.Kwahivyo, mabanki yatazamie kwa mfano, waziri wa fedha attoa muongozo wa kufuatwa katika biashara zao.

Isitoshe, hata mishahara mikuu ya mameneja wa mabanki sasa yaweza ikapunguzwa.Na iwapo serikali ikishirikiana na banki kununua hisa, halafu baadae banki ikiwa katika hali bora baada ya kujikomboa kutoka madeni yake ya zamani yalioiumbisha, serikali inaweza ikadai kurejeshwa fedha zake tena kikamilifu ilizochangia kuinua banki hiyo.

Hatahivyo, mpango huo uliotungwa kuyaokoa mmabanki nchini Ujerumani ,umezusha mjadala mpya jinsi ya kuimarisha hazina ya serikali.Ile shabaha kuwa na mfuko wa matumizi ya serikali usioingiza madeni ifikapo 2011, sasa haiwezi kutimizwa.Kwani, mabanki ambayo wakati huu hayaaminiani,hayana akiba kuyawezesha kuvuta pumzi na uchumi mzima unatishia kuzorota.

Kutokana na hatua zilizochukuliwa, masharti ya kuanza upya shughuli za kibanki yamepatikana kwa njia ambayo kitita cha Euro bilioni 500 kutoka mfuko wa walipakodi kitatoweka kwenye mifuko ya sirisiri ya mabanki.

Fedha za kodi ni za matumizi ya serikali bila kuhitaji ujira.Ni uzuri zaidi zikatumika kuyaokoa mabenki na kwa kufanya hivyo kuokoa nafasi za kazi kuliko kuzitumia kwa miradi mibaya .......

Mara tu mabanki yakianza enzi mpya , hatua za kujenga na kuusafisha mfumo mzima wa mabanki, zitachukua muda kukamilika. Hapo tena ndipo mabanki hayo yatakapopaswa kujibu maswali magumu ilikuaje hali kufikia ilipofika ?