Ujerumani, nchi zingine zaadhimisha Siku ya Wanawake Duniani
8 Machi 2026
Matangazo
Sherehe na harakati mbalimbali zimeshuhudiwa katika mji mkuu Berlin ambapo watetezi wa haki za wanawake wamelalamikia kuhusu haki na usawa wa kijinsia.
Waziri wa Ujerumani anayehusika na masuala ya Familia, Wanawake na Wazee Karin Prien amesema Ujerumani imepiga hatua katika suala la usawa kati ya wanawake na wanaume ambalo amesema ni hitaji la kikatiba, lakini akasisitiza kuwa hali hiyo inaweza kuboreshwa.
Kwa upande wa Afrika, Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amesema maadhimisho ya siku hii yanakumbusha wajibu muhimu kwa vizazi vya sasa na vijavyo wa kuendelea kupanga na kutekeleza mipango ya kumwezesha mwanamke kama juhudi za kukomboa familia, jamii na taifa kwa ujumla.