1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ujerumani na India zakubaliana kukuza sekta zao za ulinzi

23 Aprili 2026

Waziri wa Ulinzi wa Ujerumani Boris Pistorius na waziri mwenzake wa India Rajnath Singh wamesaini mpango wa vifungu 10 unaolenga kuimarisha ushirikiano katika sekta ya ulinzi na kuikuza sekta hiyo.

https://p.dw.com/p/5Cg6K
Pistorius na waziri mwenzake wa ulinzi wa India Singh watembelea kampuni ya ujenzi wa manowari ya TKMS
Ujerumani na India zimesaini mpango wa vifungu 10 unaolenga kuimarisha ushirikiano katika sekta ya ulinzi na kuikuza sekta hiyo.Picha: Christian Charisius/dpa/picture alliance

Mawaziri hao walitembelea kampuni ya ujenzi wa manowari ya TKMS katika mji wa bandari wa Kiel, kaskazini mwa Ujerumani pamoja na ujumbe wa India. Waliikagua nyambizi ya Jeshi la Wanamaji la Ujerumani ya Daraja la 212A. Waziri wa Ulinzi wa Ujeruamani Pistorius alisisitiza kwamba kusainiwa kwa mpango huo kutapeleka ushirikiano wa sekta ya ulinzi "katika hatua nyingine."

India pia inapanga kutengeneza manowari sita zenye thamani ya euro bilioni 8 huko Mumbai kwa ushirikiano na kampuni ya Ujerumani ya TKMS. Makubaliano hayo yanatarajiwa ndani ya miezi michache ijayo. Kulingana na takwimu za hivi punde kutoka taasisi ya kimataifa ya utafiti wa amani ya SIPRI, India inachukuliwa kuwa nchi inayoagiza silaha kwa wingi zaidi duniani.