1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ujerumani kupiga marufuku Kanisa la Scientology

8 Desemba 2007
https://p.dw.com/p/CZ5U

BERLIN

Mawaziri wa mambo ya ndani wa serikali ya shirikisho na wale wa mikoa wa Jamhuri ya Ujerumani wametangaza kwamba Kanisa la Scientology liko kinyume na katiba.

Hatua hiyo sasa inafunguwa njia ya uwezekano wa kupigwa marufuku kwa kanisa hilo nchini Ujerumani.Mawaziri hao wamewataka makachero wa ndani ya nchi kukusanya habari juu ya harakati za kanisa hilo ambapo kutapelekea kuanzishwa kwa tume ya uchunguzi mwaka ujao.

Ujerumani haitambui Scientology kuwa ni dini na inaiona kama ni kundi linalotumia kisingizio cha kuwa kanisa kwa nia ya kujitafutia fedha.

Kanisa hilo linapinga maoni hayo.