Udondozi wa magazeti ya Ujerumani | Magazetini | DW | 02.10.2006
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages

Magazetini

Udondozi wa magazeti ya Ujerumani

Kansela wa Ujerumani Bi Angela Merkel amewataka wakaazi wa magharibi mwa Ujerumani wajihushishe zaidi katika kulijenga eneo la mashariki, huku siku ya muungano wa Ujerumani ikiadhimishwa kesho. Meneja wa kampuni ya Siemens hapa Ujerumani Klaus Kleinfeld akosolewa baada ya kampuni ya BenQ kufilisika.

Likituanzia gazeti la Tagesspiel la mjini Berlin limeandika; asilimia 25 pekee ya wajerumani wanaoishi eneo la mashariki wameridhika na jinsi demokrsaia inavyofanya kazi. Katika eneo la magharibi ni kila mjerumani mmoja katika kila wajerumani wawili. Kwamba wapiga kura wanauezo wa kulazimisha uaminifu na hali ya kumaanisha. Na hili sio jambo wanalohitaji kufunzwa na chama cha NPD.

Katika demokrasia matatizo ya kisiasa yanahitaji bidii za kisiasa na kuwa tayari kuyatatua. Uongo hautakikani. Pengine huu ni wakati mwafaka wa kulikumbuka jambo hili, miaka 16 tangu Ujerumani kuungana.

Mhariri wa gazeti la Märkische Allgemeine la mjini Potsdam anasema siku ya muungano wa Ujerumani inaendelea kuwa siku ya takwimu na ya kawaida tu. Ukweli ni kwamba ndoto ya kujenga viwanda katika eneo la mashariki mwa Ujerumani haijatimia. Mpaka leo wafanyakazi wa miji ya mashariki bado wanakabiliana na mabadiliko katika soko la kimataifa kama vile wale wa mjini Munich au Rüsselsheim.

Na hata chama cha PDS si chama cha eneo la mashariki pekee, bali kimo njiani kupanua mbawa zeka katika maeneo yote ya Ujerumani na kuwa nguzo ya upinzani. Mhariri anasema sababu ya kusherehekea Oktoba 3 inabakia pale pale: kufanya juhudi zaidi kuliungaisha taifa katika siku za usoni badala ya kuwa na taifa lililogawanyika.

Gazeti la Heilbronner Stimme linasema mengi yamefanyika tangu mwaka wa 1990. na wajerumani wa eneo la mashariki na wale wa magharibi wanatakiwa kujivunia ufanisi uliofikiwa. Muungano wa Ujerumaji ni jambo lililo wazi kama ilivyokuwa wakati nchi hii ilipokuwa zamani imegawanyika katika eneo la mashariki na magharibi. Kujumuishwa kwa majimbo matano mapya katika shirikisho la Ujerumani lilikuwa jambo la ufanisi bila kujali misingi ya wakaazi.

Mhariri wa gazeti la Neue Osnabrücker anasema miito hapa, sherehe pale. Haya hayatakosekana hapo kesho wakati wa kuadhimisha siku ya muungano wa Ujerumani. Kansela Angela Merkel tayari katika ujumbe wake amewatolea mwito wajerumani wa eneo la magharibi wajitolee zaidi kulijenga eneo la mashariki.

Lakini hatafanikiwa kwa sababu kwa nini watu wachukue jukumu linalofanywa tayari na serikali. Mabilioni ya fedha yametolewa kulijenga aneo hilo lakini mpaka leo hali bado haijakuwa nzuri. Watu hawatakuwa tayari kuongeza michango yao, ila kwa mtazamo huu kodi zote za juu zinatakiwa kwanza zipunguzwe.

Mada nyengine iliyoripotiwa ni shinikizo linaloikabili kampuni ya Siemens kufuatia kufilisika kwa kampuni ya Taiwanya BenQ hapa. Wahariri wamemkosoa vikali kiongozi wa kampuni ya Siemens, Klaus Kleinfeld.

Gazeti la Abendzeitung la mjini Munich linasema kuuzwa kwa kitengo cha kutengeza simu za mkono cha kampuni ya Siemens kwa kampuni ya BenQ ni hasara kubwa. Hii kwa sababu bwana Kleinfeld hakutilia maanani tangu awali juhudi za kulinda nafasi za ajira. Mhariri anasema hali ya kampuni ya BenQ ni mbaya, lakini bwana Kleinfeld kwa sasa ni meneja mbaya zaidi kikazi na hata kibinadamu.

 • Tarehe 02.10.2006
 • Mwandishi Josephat Charo
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/CHUn
 • Tarehe 02.10.2006
 • Mwandishi Josephat Charo
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/CHUn