Uchambuzi wa magazeti ya Ujerumani | Magazetini | DW | 01.03.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Magazetini

Uchambuzi wa magazeti ya Ujerumani

Mada mbili zilizogonga vichwa vya habari katika magazeti mengi ya Ujerumani leo hii ni mradi wa kufanyia ukarabati kampuni la ndege la Ulaya Airbus na kupunguka kwa idadi ya watu wasio na ajira katika mwezi wa Februari.

Tunaanza na gazeti la ALLGEMEINE ZEITUNG kutoka Mainz,linalosema:

“Mambo yangeweza kuwa mabaya zaidi.Lakini hata hivyo, ukweli wa mambo unashtusha na unahamakisha vile vile,kwani mradi huo wa ukarabati si kingine isipokuwa kufutilia mbali nafasi 10,000 za kazi. Kutoka idadi hiyo 3,700 ni nchini Ujerumani.“

BERLINER ZEITUNG nalo linasema:

“Kampuni la Airbus katika mradi wake wa ukarabati,linataka kufuta nafasi elfu kadhaa za kazi.Kiuchumi,mtu atadhania kuwa hilo ni jambo la mantiki lakini ukweli ni mwingine,kwani jinsi orodha ya maagizo ilivyo ndefu,kampuni la Airbus linashindwa hata kutimiza maagizo ya ndege zake. Mwanauchumi ye yote yule angeshauri kuongeza mwendo wa kutengeneza ndege hizo ili kuweza kutimiza maagizo ya wateja.“

Gazeti la MAIN-ECHO kutoka Aschaffenburg likiendelea na mada hiyo hiyo linasema:

“Matatizo ya Airbus na hasa kuhusu mradi wake wa hadhi wa ndege ya A380,hayasababishwi sana na gharama kubwa za kutengeneza ndege hiyo ya fahari,bali ni kwa sababu ya makosa ya uongozi,miundombinu ya kijinga na pia serikali kuingilia kati mara kwa mara.Na sababu hiyo ya mwisho ndio itakayoleta matatizo zaidi katika siku zijazo.Ujerumani na Ufaransa kamwe hazitokuwa na ushirkiano wa maelewano kuhusu suala la Airbus.Litakuwa jambo la busara kwa serikali kuacha kuingilia kati kampuni hilo la ushirikiano wa nchi za Ulaya.“

Sasa tunapindukia mada nyingine iliyoshughulikiwa na magazeti ya Ujerumani leo hii yaani kupunguka kwa idadi ya watu wasio na ajira katika mwezi wa Februari.NORDBAYERISCHE KURIER kutoka Bayreuth linasema:

“Katika historia ya Shirikisho la Jamhuri ya Ujerumani,idadi ya watu wasio na ajira haijawahi kupunguka katika kipindi cha mwaka mmoja,kama ilivyotokea mwezi wa Februari.Hiyo ni rekodi nzuri inayofaa kungángániwa kwa muda fulani.Wakati huo huo katika majadiliano yajayo kuhusu mishahara,pande zote husika zinapaswa kutoa madai yanayoweza kutekelezwa ili watu wasio na ajira wasije kuachwa nyuma.Idadi ya watu wasio na kazi inapopunguka,basi hata idadi ya wale walio na uwezo wa kununua huongezeka.Hiyo ni hali ya uchumi iliyo bora kabisa.Soko la ajira ndio limefufuka lamalizia NORDBAYERISCHE KURIER.