Uchaguzi wa rais nchini Guinea | Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili | DW | 07.11.2010
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Timu Yetu

Uchaguzi wa rais nchini Guinea

Duru ya pili ya uchaguzi wa rais inafanyika leo, baada ya kuahirishwa mara kadhaa.

default

Mgombea urais nchini Guinea, Alpha Conde.

Raia nchini Guinea wameombwa kubakia shwari watakapopiga kura hii leo katika duru ya pili ya uchaguzi wa rais ulioahirishwa mara kadhaa. Hii ni mara ya kwanza kwa raia nchini Guinea kumchagua rais wa kiraia katika uchaguzi wa kidemokrasia wa kwanza baada ya zaidi ya miaka 50.

Duru hiyo ya pili ya uchaguzi inawapambanisha wagombea wanatoka katika makabila mawili makubwa nchini humo na hiyo imezusha ghasia na hali ya kutoaminiana. Hata hivyo Cellou Dalein Diallo na Alpha Conde walijitokeza pamoja na kutoa mwito wa utulivu katika taifa hilo la Afrika Magharibi. Kumekuwepo na uhasama katika pande zote mbili tangu kufanyika kwa duru ya kwanza ya uchaguzi Juni 27 ambapo hakuna aliejitokeza mshindi.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com