Uchaguzi Pakistan | Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili | DW | 18.02.2008
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages

Timu Yetu

Uchaguzi Pakistan

Raia wajitokeza licha ya vitisho vya mabomu

default

Wafuasi wa waziri mkuu wa zamani wa Pakistan, Nawaz Sharif, wakiwa na bendera pamoja na mabango wakati wa mkutano wa chama chake cha the Pakistan Muslim League-N Party katika sehemu ya Chakwal, Pakistan Jumatano Feb. 13, 2008.

Raia mamia kadha wa Pakistan,licha ya vitisho vya mabomu na risasi walijitokeza kwa wingi leo kushiriki katika uchaguzi wa wabunge ambao utaamua majaliwa ya Rais Perves Musharraf-anaeegemea Marekani.


Raia mamia kadhaa wa Pakistan,licha ya vitisho vya mabomu na risasi walijitokeza kwa wingi leo kushiriki katika uchaguzi wa wabunge ambao utaamua majaliwa ya Rais Perves Musharraf-anaeegemea Marekani.


Matokeo ya uchaguzi wa bunge wa leo nchini Pakistan hayajulikana baado.


Uchaguzi wa leo ulikuwa,utumike kama daraja kutoka katika mfumo mmoja wa kijeshi,wa miaka minane hadi ule wa kidemokrasia.Hata hivyo umefanyika wakati kukiwa na wingu la ghasia mkiwemo mauaji ya waziri mkuu wa zamani Benazir Bhutto.Hatua muafaka zilichukuliwa na serikali ya Mushsrraf za kuweka ulinzi mkali na pia kutoa onyo kali dhidi ya watakao jaribu kufanya vurugu.


Bila shaka washirika wa nchi za magharibi wakiongozwa na Marekani katika kile kinachoitwa vita dhidi ya ugaidi wanauangalia kwa jicho kali,katika jamhuri ilio na silaha za Nuklia huku kukisikika mapema miito ya viongozi wa upande wa upinzani wa kukataa matokeo ikiwa kutatokea mizengwe.


Mbali na hayo yote wananchi walijitokeza kwa wingi baada ya awali kujikokota kuwasili katika vituo vya kupigia kura katika baadhi ya vituo nchini humo saa tatu kabla ya vituo kufungwa saa kumi na moja jioni saa za Pakistan.Awali afisa mmoja wa tume ya uchaguzi nchini humo alisema kuwa asili mia ya wapigajikura iliojitokeza leo ni 35 ya watu millioni 81 ya watu wote ambao walijiandikisha kupiga kura.


Maafisa wanasema idadi ya wapiga kura haikuwa kubwa labda kwa sababu ya kuhofia usalama wao licha ya askari jeshi wapatao laki nane, kushika doria katika maeneo kadhaa.


Matokeo yote yanatarajiwa kujulikana hapo kesho japo ya mwanzo yalitegemewa kuanza kutolewa saa nne za usiku saa za Pakistan.


Kuhusu hali ilivyokuwa wakati wa uchaguzi,afisa moja wa tume ya uchaguzi,katibu mkuu wa tume hiyo-Kanwar Dilshad- amenukuliwa na vyombo vya habari vya kigeni akisema kuwa uchaguzi umemalizika vizuri bila ya visa vibaya.


Kwa upande mwingine maafisa wanasema watu 14 wameuawa katika ghasia ambazo zilianza katika mkesha wa uchaguzi.


Musharraf, aliechukua madaraka baada ya kupindua serikali mwaka wa 1999,alivua ngwanda la kijeshi na hivyo kugawa madaraka ya jeshi kwa mtu mwingine mwezi Novemba mwaka jana.Aliomba kuwepo na maridhiano na kuvionya vyama vyote kukubal,i kwa mwoyo mmoja, matokeo ya uchaguzi wa leo.Baada ya kupiga kura yake mjini Rawalpindi,rais Musharraf alihutubia taifa kupitia teklevisheni akisema ,yeyote atakae shinda-yeye kama rais atashrikiana nae.

lakini rais Musharraf anakabiliwa na kuondolewa madarakani ikiwa matokeo ya uchaguzi yatawaleta bungeni wapinzani wake.Na ikiwa ataweza kuvuka tisho hilo,lakini madaraka yake yatapunguzwa.


Musharraf,aliekuwa Jenerali wa kijeshi,anachukuliwa na Marekani kama mshirika mkuu katika vita dhidi ya Al Qaida na wapiganaji wa Kitaliban walioko katika maeneo ya kikabila ya mpaka kati ya Pakistan na Afghanistan.


Kura za maoni ya awali zilionyesha kuwa chama cha Bhutto cha Pakistan People's Party-PPP- kingepata ushindi na kufuatiwa na kile cha waziri mkuu wa zamani Nawaz Sharif huku kile kinachomuunga mkono Musharraf cha Pakistan Muslim League-Q (PML-Q) kuchukua nafasi ya tatu.

 • Tarehe 18.02.2008
 • Mwandishi Kalyango, Siraj
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/D9L4
 • Tarehe 18.02.2008
 • Mwandishi Kalyango, Siraj
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/D9L4
Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com