Tume ya uchaguzi Georgia yasema rais Mikhail ndie mshindi | Habari za Ulimwengu | DW | 13.01.2008
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Tume ya uchaguzi Georgia yasema rais Mikhail ndie mshindi

TIBLIS:

Maelfu ya wafuasi wa upande wa upinzani wameandamana katika mji mkuu wa Tiblis,kupinga matokeo ya uchaguzi wa urais uliofanyika Januari 5. wandamanaji hao wanadai kuwa kulitokea danganyifu uliopeleka rais Mikhail Saakashvili,anaeegemea Marekani, kurejea madarakani. Wandaamanaji,licha ya baridi kali,walipitia barabara za mjini Tiblis wakipiga makelele kumpinga Saakashvili na kutaka kura kuhesabiwa tena. Matokeo ya mwisho ambayo yametolewa leo jumapili yamempa Saakashvili ushindi wa zaidi y asili mia 53 ya kura zote zilizopigwa,huku mpinzani mkuu Levan Gachechiladze-(Gasheshiladze) kushika nafasi ya pili kwa kupata asili mia zaidi ya 25 ya kura zilizopigwa.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com