Migogoro
Marekani yaikosoa NATO kwa kuitenga katika mzozo wa Iran
9 Aprili 2026
Matangazo
Donald Trump pia amezikosoa nchi wanachama wa NATO kwa kwa kukataa kutoa msaada wa kijeshi katika suala la Mlango Bahari wa Hormuz. Ameyatoa malalamiko hayo mbele ya Katibu Mkuu wa Jumuiya hiyo Mark Rutte walipofanya mazungumzo Jumatano kwenye Ikulu ya Marekani, White House.
Mkuu wa NATO akiri baadhi ya nchi zilishindwa kutimiza wajibu
Aidha Katibu Mkuu Rutte amejibu kuwa anatambua kuwa badhi ya mataifa yalishindwa kutimiza wajibu wao lakini washirika hao wamekuwa wakisaidia na kuhakikisha kuwa wanatimiza ahadi zao.
Mgogoro ndani ya NATO kati ya Marekani na Washirika wa Ulaya umezidisha wasiwasi ndani ya Jumuiya hiyo huku wachambuzi wakionya kuwa uko mashakani kusambaratika