Tishio la kigaidi Ujerumani | Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili | DW | 18.11.2010
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Timu Yetu

Tishio la kigaidi Ujerumani

Waziri wa ndani wa Ujerumani Thomas De Maiziere aonya kuhusu tishio la kigaidi nchini.

default

Waziri wa ndani wa Ujerumani Thomas de Maiziere.

Waziri wa ndani wa Ujerumani Thomas De Maiziere ameonya kwamba maafisa wa usalama wana ushahidi mpya na wa kuaminika kwamba wanamgambo wa kiislamu  wanapanga shambulio la kigaidi  nchini Ujerumani kufikia mwishoni mwa mwezi huu.

Waziri Maiziere amewaambia waandishi wa habari katika mkutano nao uliofanyika mjini Berlin hapo jana, kwamba kutokana na hilo, anazidisha kiwango cha tahadhari kwa shambulio la kigaidi.

De Maiziere amesema ameamrisha kuzidishwa marudufu uwepo wa maafisa wa polisi wanao onekana na wa siri nchini. Amesema taarifa hizo zimepokewa kutoka Yemen na amewaomba raia kuwa waangalifu.

Razzia Islam München

Maafisa wa polisi nchini Ujerumani.

Vyombo vya habari vya Ujerumani vimezinukuu duru za usalama vikisema kwamba  hadi magaidi wanne wenye itikadi kali za dini ya kiislamu wanaelekea Ujerumani kutekeleza mashambulio.

Mwandishi: Maryam Dodo Abdalla/DPAE

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com