Tel Aviv. Hamas kusakwa zaidi na majeshi ya Israel. | Habari za Ulimwengu | DW | 28.05.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Tel Aviv. Hamas kusakwa zaidi na majeshi ya Israel.

Waziri mkuu wa Israel Ehud Olmert amesema kuwa msako dhidi ya kundi lenye msimamo mkali wa Kiislamu la Hamas utaendelea.

Olmert ametoa maelezo hayo katika kikao cha baraza la mawaziri , saa chache baada ya raia mmoja wa Israel kuuwawa kwa kombora lililorushwa na Wapalestina dhidi ya mji wa Sderot, ambapo kundi la Hamas limedai kuhusika.

Mtu huyo mwenye umri wa miaka 36 ni raia wa pili wa Israel kuuwawa katika mashambulizi ya maroketi ya Wapalestina tangu ghasia za hivi sasa kuanza kiasi cha wiki mbili zilizopita.

Zaidi ya Wapalestina 40 wameuwawa katika mashambulizi ya anga ya Waisrael.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com