TAIPEI : Gwaride la kijeshi laadhimisa siku ya taifa | Habari za Ulimwengu | DW | 10.10.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

TAIPEI : Gwaride la kijeshi laadhimisa siku ya taifa

Ikiwa ni sehemu ya sherehe za Siku ya Taifa Taiwan imekuwa na gwaride la kijeshi lililosanifiwa kuonyesha ubavu wake kwa nchi jirani ya China.

Ndege za kivita za F-16 na helikopta ziliuzunguka mji mkuu wa Taipei na makombora kadhaa yaliotengenezwa ndani ya nchi yalionyeshwa hadharani.Katika hotuba ilioonyeshwa kwenye televisheni Rais Chen Shui Bian amekuita kujiimarisha kijeshi kwa China kuwa ni tishio kwa dunia na ameitaka Jamhuri ya Watu China itambuwe haki ya kujitawala kwa nchi hiyo.Pia amesema serikali yake itaendelea kupigania uwanachama wa Umoja wa Mataifa.

Taiwan imetolewa kwenye Umoja wa Mataifa tokea kuingia kwa China hapo mwaka 1971.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com