Taasisi ya Goethe ni miongoni mwa taasisi tano za Ulaya zilizotunukiwa zawadi ya mwaka huu ya Prinz-von-Asturien | Habari za Ulimwengu | DW | 02.06.2005
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Habari za Ulimwengu

Taasisi ya Goethe ni miongoni mwa taasisi tano za Ulaya zilizotunukiwa zawadi ya mwaka huu ya Prinz-von-Asturien

Madrid:

Taasisi ya Ujerumani- Goethe pamoja na taasisi nyengine tano za Ulaya,zimetunzwa zawadi ya mwaka huu ya Prinz-von-Asturien.Habari hizo zimetangazwa na jopo la mawakili la taasisi hiyo inayohimiza kuimarishwa mawasiliano na kubadilishana taaluma.Mbali na taasisi ya Ujerumani-Goethe,nyengine ni British Council ya Uengereza,taasisi ya Cervantes ya Hispania,Societa Dante Alighieri ya Italy,Alliance Francaise ya Ufaransa na taasisi ya Ureno Camaoes.Kwa kutunukiwa zadai hiyo,taasisi ya Prinz von Asturien imetaka kushukuria juhudi za taasisi hizo katika kutoa mafunzo ya lugha na kueneza fasihi na maadili ya Ulaya kote ulimwenguni.Zawadi hiyo itatolewa october 21 ijayo katika mji wa kaskazini wa Hispania Oviedo.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com