1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Sudan ya Kusini yasheherekea uhuru wake

Miraji Othman9 Julai 2011

Vifijo na nderemo mjini Juba

https://p.dw.com/p/11sAU
majeshi ya usalama ya Sudan ya Kusin yajitayarisha kwa gwaride la sherehe za uhuru huko JubaPicha: ap

Leo taifa jipya la Sudan ya Kusini limezaliwa baada ya vita vya miaka mingi kutaka sehemu hiyo ijitenge na Sudan. Sherehe na nderemo zimehanikiza katika mji mkuu wa Juba ambapo Salva Kiir ameapishwa  kuwa rais wa kwanza wa nchi hiyo. Mgeni  rasmi katika sherehe hizo ni Rais wa Sudan, Omar al-Bashir, ambaye anatakiwa na mahakama ya kimataifa ya uhalifu kukabiliana na mashtaka dhidi ya ubinadamu na mauaji ya halaiki huko Dafur.

Nimeungana sasa na mwandishi wetu wa Deutsche Welle huko Juba, Leylah Ndinda....Hebu tuelezee Leylah vipi siku ya leo ya kihistoria inavoadhimishwa