Spika wa bunge la Marekani akutana na Dalai Lama | Habari za Ulimwengu | DW | 21.03.2008
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Habari za Ulimwengu

Spika wa bunge la Marekani akutana na Dalai Lama

DHARAMSHALA:

Spika wa baraza la wawakilishi la Marekani amekutana leo na kiongozi wa kidini wa Tibet katika makao yake kaskazini mwa India.Nancy Pelosi ameielezea jinsi China ilivyozima maandamano ya tibet kama changamoto kwa uhuru wa kujiamulia .Nancy Pelosi ndie afisa wa ngazi ya juu wa kwanza kufanya mazungumzo na Dalai Lama tangu kuzuka kwa ghasia katika jimbo la Tibet anakotoka Dalai Lama.

Mkutano huu unafanyika wakati viongozi wa China na Tibet wakiendelea kubishana kuhusu idadi ya wahanga wa mkong'oto wa China wakati inazima maandamano katika eneo la Tibet.Wakuu wa China wanasema waliwapiga risasi na kuwajeruhi waandamanji wanne tu mwishoni mwa juma.Hata hivyo wanawalaumu waandamanaji kwa kuwauwa raia 13 wakati ghasia zilipolipuka katika mji wa jimbo hilo wa Lhasa,Ijuma ya wiki iliopita.Lakini wao Watibet wanaoishi uhamishoni wanadai kuwa vikosi vya usalama vya China viliwauwa takriban watu 100 wiki iliopita.

Kwa mda huohuo wakuu wa China wametoa picha katika mtandao wa Internet za watu 21 inayowatafuta kwa kuhusika na ghasia za hivi majuzi katika jimbo la Tibet.Aidha Beijing imepeleka wanajeshi zaidi katika maeneo ya Tibet ya China magharibi.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com