SEVILLE: Russia yapinga hatua ya Marekani kuweka mitambo ya ulinzi, Ulaya Mashariki. | Habari za Ulimwengu | DW | 10.02.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

SEVILLE: Russia yapinga hatua ya Marekani kuweka mitambo ya ulinzi, Ulaya Mashariki.

Waziri wa Ulinzi wa Russia, Sergei Ivanov, amesema hakuna haja ya Marekani kuweka mitambo ya ulinzi ya kukinga makombora katika eneo la mashariki mwa Ulaya.

Waziri huyo alikuwa akizungumza na waandishi wa habari mjini Seville, Uhispania baada ya mkutano wa mawaziri wa Ulinzi wa Umoja wa Ulaya.

Sergei Ivanov alisema Poland na Jamhuri ya Czech hazimo katika eneo zuri la Marekani kujikinga na shambulio kutoka Korea Kaskazini au Iran.

Waziri wa Ulinzi wa Marekani, Robert Gates, amesema haoni sababu za Russia kupinga mpango huo wa ulinzi wa Marekani.

Waziri Sergei Ivanov alisema Russia itarekebisha mifumo yake ya ulinzi kuhakikisha kwamba itaendelea kutenda kazi ipasavyo.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com