1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Safari za ndege zafutwa katika uwanja wa ndege Munich

3 Oktoba 2025

Zaidi ya safari 17 za ndege zimefutwa katika uwanja wa ndege wa Munich, Ujerumani, kufuatia kuonekana kwa droni katika anga ya uwanja huo.

https://p.dw.com/p/51RL1
Ujerumani | München 2025 | Uwanja wa ndege wa Munich | Franz Josef Strauß
Ndege ya Lufthansa inapaa kutoka uwanja wa Ndege wa MunichPicha: Michael Bihlmayer/IMAGO

Hali hiyo imeathiri abiria 3,000 huku ndege nyingine 15 zilizotarajiwa kutua katika uwanja huo zikielekezwa katika viwanja vya ndege vya Stuttgart, Nuremberg, na Frankfurt.

Kwa mujibu wa taarifa ya usimamizi wa uwanja huo, tukio hilo limeongeza taharuki ya kiusalama, hasa ikizingatiwa kuwa limetokea siku chache tu baada ya viwanja vya ndege vya Denmark na Norway kufungwa kwa muda kutokana na matukio ya aina hiyo ya droni kuonekana katika anga ya nchi hizo.

Mji wa Munich tayari ulikuwa katika hali ya tahadhari mapema wiki hii, baada ya tamasha maarufu la Oktoberfest kusitishwa kwa muda kufuatia tishio la bomu na kugunduliwa kwa vilipuzi katika jengo la makaazi kaskazini mwa mji huo.

Viongozi wa Umoja wa Ulaya wameunga mkono pendekezo la kuimarisha ulinzi wa anga wa nchi wanachama dhidi ya tishio la droni, hasa zile zinazodaiwa kuwa za Urusi.