1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Denmark yataja tukio la ndege za droni kuwa shambulio baya

23 Septemba 2025

Waziri Mkuu wa Denmark Mette Frederiksen amekitaja kitendo cha idadi kubwa ya droni zilizoruka katika uwanja wa ndege wa Copenhagen kwa masaa kadhaa kuwa ni shambulio baya zaidi kwa miundombinu muhimu ya nchi hiyo.

https://p.dw.com/p/50yEN
Denmark Copenhagen 2025 | Mette Frederiksen akizungumza na waandishi wa habari kuhusu droni kwenye uwanja wa ndege
Waziri Mkuu wa Denmark Mette Frederiksen Picha: Emil Nicolai Helms/Ritzau Scanpix/picture alliance

Waziri Mkuu wa Denmark Mette Frederiksen amekitaja kitendo cha idadi kubwa ya ndege za droni zilizoruka katika uwanja wa ndege wa Copenhagen kwa masaa kadhaa kuwa ni shambulio baya zaidi kwa miundombinu muhimu ya nchi hiyo. Viwanja vya ndege katika miji ya Copenhagen na Oslo, vilifunguliwa tena mapema leo Jumanne, saa kadhaa baada ya droni kugundulika katika anga zake na kusababisha dazeni ya safari za ndege kuhamishiwa katika viwanja vingine au kusitishwa. Alipoulizwa ikiwa anashuku Urusi imehusika, amesema; "Kwa hakika siwezi kukataa kwa njia yoyote kwamba ni Urusi. Tumeona ndege za droni zikiruka Poland ambazo hazikupaswa kuwepo. Tumeona shughuli hizo Romania na ukiukaji wa anga ya Estonia. Kumekuwa na droni Denmark na inaonekana pia zimeruka Oslo na kwingineko huko Norway. Kwa hivyo naweza kusema tu kwamba, hili ni shambulio kubwa kwa miundombinu muhimu ya Denmark." Msemaji wa Ikulu ya Urusi Kremlin Dmitry Peskov amekanusha madai hayoya Denmark akisema hayana msingi.