Migogoro
Urusi yakanusha ndege zake kuingia katika anga ya NATO
22 Septemba 2025
Matangazo
Ijumaa, Estonia ambayo ni mwanachama wa Jumuiya ya NATO ilisema ndege tatu za kijeshi za Urusi ziliingia kwenye anga yake na kudumu kwa dakika 12 kabla ya kutolewa nje zikisindikizwa na ndege za Jumuiya hiyo.
Urusi kupitia msemaji wake Peskov imesema madai ya Estonia hayana msingi na ni mwendelezo wa sera yake ya kuongeza mivutano na kuanzisha uchokozi. Kwa upande wa NATO, mabalozi wake watafanya mazungumzo Jumanne baada ya Estonia kuitisha majadiliano yanayohusu tukio hilo.