Ramallah.Mizinga mitatu ya Israel yapiga katika nyumba huko Gaza. | Habari za Ulimwengu | DW | 09.11.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Ramallah.Mizinga mitatu ya Israel yapiga katika nyumba huko Gaza.

Chama tawala cha Wapalestina Hamas na makundi ya wanaharakati yenye mafungamano na chama hicho vimetowa mwito kwa waarabu na waislamu, kushambulia maeneo ya masilahi ya Marekani katika Mashariki ya kati, ikiwa ni kama kulipiza kisasi dhidi ya mauaji yanayofanywa na Israel Kaskazini mwa Gaza.

Kiasi ya Wapalestina 18 wameuwawa na 40 wamejeruhiwa wakati mizinga mitatu ilipopiga nyumba Mashariki mwa viunga vya kazkazini mwa Gaza katika mji wa Beit Hanoun mapema jana.

Israel imekiri kuwa kuwa mashambulizi hayo yalikuwa ni ya bahati mbaya na imeelezea masikitiko yake kwa kosa hilo.

Shambulio hilo limelaumiwa na Umoja wa Ulaya EU na Marekani.

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limeitisha mkutano hii leo kujadili kuhusu maafa mapya yanayoendelezwa na Israel hivi sasa.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com