RAMALLAH: Waziri wa mambo ya nchi za nje wa Marekani, Condoleeza Rice, aendelea na ziara yake Mashariki ya Kati. | Habari za Ulimwengu | DW | 14.01.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

RAMALLAH: Waziri wa mambo ya nchi za nje wa Marekani, Condoleeza Rice, aendelea na ziara yake Mashariki ya Kati.

Waziri wa mambo ya nchi za nje wa Marekani, Condoleezza Rice amewasili mjini Ramallah kushauriana na Rais wa Palestina, Mahmoud Abbas katika siku ya pili ya ziara yake ya juma moja Mashariki ya Kati.

Bi Condoleezza Rice jana mjini Jerusalem alishauriana na Waziri wa mambo ya nchi za nje wa Israil Tzipi Livni ambapo alitoa wito wa kuwa na suluhisho mwafaka la mzozo kati ya Israil na Wapalestina.

Marekani imekuwa ikishinikizwa na washirika wake kutoka Ulaya na pia mataifa ya Kiarabu kufufua mashauriano ya amani ya Mashariki ya Kati.

Baadaye hivi leo, Bi Condoleezza Rice anatarajiwa kuitembelea Jordan kabla ya kukutana na Waziri Mkuu wa Israil, Ehud Olmert kesho.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com