1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Migogoro

Zelensky ayasifu mazungumzo ya kutafuta amani Ukraine

25 Januari 2026

Rais wa Ukraine, Volodymyr Zelensky amesema mazungumzo ya siku mbili yaliyolenga kuvikomesha vita nchini mwake yaliyokamilika Jumamosi mjini Abu Dhabi yamemalizika kwa mafanikio.

https://p.dw.com/p/57PkU
Ukraine bado inakabiliwa na vita karibu miaka minne tangu ilipovamiwa na Urusi
Rais wa Ukraine Volodymyr ZelenskyPicha: Ukrainian Presidential Office/AFP

Mazungumzo hayo yamewahusisha wawakilishi kutoka Ukraine, Urusi na Marekani. Zelensky kupitia chaneli yake ya Telegram amesema pande zote katika majadiliano hayo zimekubaliana kuripoti kwa viongozi wao kila kipengele cha mazungumzo na kuratibu hatua zijazo.

Kwa mujibu wa afisa wa Marekani aliyetoa sharti la kutokutajwa jina, awamu ijayo ya mazungumzo itafanyika Februari Mosi.

Jeshi, uchumi vyatawala mazungumzo

Afisa huyo amesema majadiliano yaliyokwisha yalijikita kwenye masuala mapana yanayohusu jeshi na uchumi pamoja na uwezekano wa kupata makubaliano ya kusitisha vita.

Hii ni mara ya kwanza kwa maafisa wa utawala wa Rais Donald Trump kukaa chini kwa mazungumzo na wawakilishi wa Ukraine na Urusi kama sehemu ya juhudi za kuvikomesha vita nchini Ukraine vilivyodumu kwa karibu miaka minne.