1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rais wa Palastina aisihi Israel irejee katika meza ya mazungumzo ya amani

16 Novemba 2006
https://p.dw.com/p/CCsD

Nablus:

Mwanaharakati mmoja wa kipalastina ameuwawa kufuatia hujuma za jeshi la Israel katika kambi ya waakimbizi ya Ein Beit Elma karibu na Nablus-katika ukingo wa magharibi.Kwa mujibu wa duru za usalama,kijana huyo wa miaka 25 ,alikua mfuasi wa chama cha ukombozi wa Palastina PPLF.Jana rais wa utawala wa ndani wa Palastina Mahmoud Abbas aliitolea mwito Israel irejee katika meza ya majadiliano ya amani.Katika hotuba yake kwa njia ya televisheni,rais Mahmoud Abbas ameitaka pia Israel iyahame maeneo ya Ukingo wa magharibi na Jerusalem ya mashariki.Jumla ya watu 5565 wamepoteza maisha yao,,wengi wao ni wapalastina,tangu wimbi la pili la Intifadha liliporipuka september mwaka 2000.Wakati huo huo makombora mawili ya Qassam yamefyetuliwa na wanaharakati wa kipalastina hii leo dhidi ya maeneo ya kusini mwa Israel.Hakuna lakini hasara iliyopatikana.