Rais Kagame aelekea kushinda kwa kishindo uchaguzi wa rais Rwanda
10 Agosti 2010Matangazo
Matokeo ya awali katika uchaguzi mkuu uliofanyika nchini Rwanda hapo jana yameonyesha kuwa Rais wa sasa Paul Kagame ameshinda kwa kishindo, akipata asilimia 92.9 ya kura zote. Mpinzani wake wa karibu kutoka chama cha Social Democrats Jean Damascene Ntawukuriryayo amejinyakulia asilimia 4.9, na chama chake kimetangaza kuwa kitakubali matokeo. Matokeo hayo ya awali yamepatikana baada ya kuhesabu kura kutoka wilaya 11 kati ya 30 za nchi hiyo.
Kwa maelezo zaidi huyu hapa mwandishi wetu mjini Kigali, Daniel Gakuba.
Mwandishi: Daniel Gakuba
Mhariri:Josephat Charo